Skip to content

Wadau wa uwindaji wachangia zaidi ya 6bn/-

  • Bara

NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

UWINDAJI wa kitalii umechangia kiasi cha dola za kimarekani 2,546,295 sawa na shilingi bilioni 6,606,635,525 ndani ya kipindi cha (2020/2021 to 2022/2023) kwenye miradi ya maendeleo na uendelezaji na shughuli za uhifadhi kwenye Maeneo ya Hifadhi za Wanyamapori za Jamii (WMA).

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula, alipokuwa anafungua warsha ya wadau wa uhifadhi wa tembo kwenye mifumo ikolojia inayovuka mipaka ya nchi inayo endeleo kufanyika jijini Arusha.

Kitandula alisema kuwa pamoja na mchango mkubwa unaotolewa na uwindaji wa kitalii kwenye mifumo ikolojia inayovuka mipaka ya nchi, bado ipo haja ya kuchanganua changamoto mbalimbali za matumizi ya wanyamapori.

Alisema katika warsha hiyo anategemea kuwa wadau mbalimbali wa uhifadhi watapata fursa ya kujadiliana changamoto hizo, kupeana uzoefu na mwisho watatoka na majibu ya namna bora ya kutatua changamoto zinazotokana na usimamizi wa mnyama tembo.

“Lengo ni kuhakikisha kuwa uwindaji wa tembo unafaidisha jamii lakini pia unachangia katika uhifadhi na uchumi wa Taifa kwa ujumla kupitia maandalizi miongozo na kanuni zitakazowezesha uwindaji wa tembo kwa maendeleo na uhifadhi”, alisema Kitandula.

Vilevile Kitandula kwa niaba ya Waziri wa Maliasili, Angela Kairuki alimpongeza na kumshukuru John Jackson, Raisi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Conservation Force (CF) kwa juhudi kubwa alizofanya katika kusaidia uhifadhi wa mnyama tembo kupitia uwindaji wa kitalii.