Skip to content

Habari Kuu

Most important story

Dk. Mwinyi anogesha furaha Zanzibar Heroes 

NA KHAMISUU ABDALLAH  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajia kuunda kamati maalum ya kumshauri namba bora ya kukuza soka la Zanzibar.  Dk. Mwinyi alieleza hayo katika hafla ya chalula cha mchana aliyoiandaa kwa ajili yakuwapongeza mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup timu ya Taifa ya Zanzibar,… Read More »Dk. Mwinyi anogesha furaha Zanzibar Heroes 

Dk. Mwinyi: Mazoezi kinga madhubuti ya maradhi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyiamewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kufanya mazoezi kwani ni kinga madhubutidhidi ya maradhi hasa yasioambukiza. Dk. Mwinyi aliyasema hayo katika viwanja vya Mnazimmoja Wete wakati akizungumza nawananchi waliojikeza katika bonanza la mazoezi kitaifa lililoambata na na matembeziyaliyoanzia katika uwanja wa mpira Kinyasini hadi uwanja wa Mnazimmoja, Wete Pemba. Alieleza kuwa kufanya mazoezi kutaweza kupunguza na kuondosha maradhi yasioambukizayakiwemo ya kisukari, presha pamoja na unene uliyokithiri. Aidha Dk. Mwinyi alifahamisha kuwa kuwa maradhi yasioambukiza yamekuwa yakiongezekasiku hadi siku yakilinganishwa na maradhi yanayoambukiza ambayo yalikuwa yakiongoza katikamiaka iliyopita. “Niwaombe sana ndugu wananchi, tusiache kufanya mazoezi kwani kufanya mazoezikunapelekea kujikinga na maradhi yasioambukiza,  hili tuelewe wazi”, alieleza Dk. Mwinyi. “Lakini pia niwafahamishe wana michezo wenzangu kuwa mazoezi ni afya, hivyo tuendeleekufanya mazoezi ili tuweze kuweka miili yetu sawa”, alieleza Dk. Mwinyi. Sambamba na hayo Rais Mwinyi aliwataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha hali ya amani, umoja na utulivu uliopo nchini hasa katika kipindi hiki nchi ikielekea katika uchaguzimkuu hapo baadae. “Niwaombe sana viongozi wa dini na wanasiasa kuendelee kuwahubiria wafuasi wetu juu ya umuhimu wa kuitunza amani ya nchi iliyopo”, alisisitiza Dk. Mwinyi.  Mapaema Dk. Mwinyi aliupongeza uongozi wa Chama cha Wafanya Mazoezi Zanzibar (ZABESA) kwa kuwashajihisha wananchi kuendelea kufanya mazoezi pamoja na kuendelezasiku ya mazoezi kitaifa nchini. Aidha… Read More »Dk. Mwinyi: Mazoezi kinga madhubuti ya maradhi

Dk. Mwinyi: Tutajenga uwanja mfano wa  ‘Old Traford’

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujenga uwanja mkubwawa michezo wenye hadhi ya kimataifa, kitakachotumika kwa michuano ya kimataifaikiwemo michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027. Dk. Mwinyi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na wadau wa michezo waliohudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa viwanja vya michezoMaisara (Maisara Sports Complex), mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar. “Tuna dhamira ya kweli ya kujenga uwanja wa kisasa wa… Read More »Dk. Mwinyi: Tutajenga uwanja mfano wa  ‘Old Traford’