NA MWANDISHI WETU TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema uwepowa mawakala kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kurani kielelezo cha uwazi kwenye zoezi la uboreshaji wadaftari la kudumu la wapiga kura. Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya watendajiwa daftari ngazi ya mkoa mkoani Mbeya, Mwenyekiti waINEC, Jaji Jacobs Mwambegele, alisema pamoja nakuhakikisha zoezi linafanyika kwa uwazi mawakala haopia watasaidia kuwatambua wananchi wanaoombakuandikishwa. “Wakati wa uboreshaji wa daftari mawakala wa vyama vyasiasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikishawapiga kura. Jambo hili ni muhimu kwani litasaidia kuletauwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala haowatasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyokupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima,” alisema. Aliongeza kuwa mawakala hao hawaruhusiwi kuwaingiliawatendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yaovituoni. Akizungumza wakati wa kufungua mkutano kama huomkoani Iringa, Makamu Mwenyekiti wa INEC, Jaji(Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk, alisema katikakuhakikisha zoezi hilo linakuwa la uwazi, Tume imetoakibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshajiwa daftari kwa asasi za kiraia 157 na asasi za kiraia 33 kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hilo. “Ni muhimu kutoa ushirikiano kwa asasi hizo zitakapofikakwenye maeneo yenu kwa ajili ya kutekeleza majukumuyao. Tume itawapa vitambulisho kwa urahisi wakuwatambua,” alisema Jaji Mbarouk. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi yauboreshaji wa daftari mkoani mbeya, iringa na mkoa wadodoma kwenye halmashauri ya wilaya ya mpwapwaambapo uboreshaji utafanyika kwa siku saba kuanziaDisemba 27 Januari 02, 2025.